Nyimbo za Sayansi! | Ubongo Kids - elimu burudani wa watoto

Published: 23 June 2017
on channel: Ubongo Kids Kiswahili
4,734,783
6.8k

Imba nyimbo za sayansi na wakina Mama Ndege, Anko T, Kibena, Kiduchu, Koba, Baraka na Amani! Jifunze kuhusu nishati ya sauti, mwanga, mwili, ukuaji, uzito na ujazo kupitia nyimbo za Ubongo Kids!

--

Jamani! Mwaka huu, Ubongo Kids ni ZAIDI ya hisabati na sayansi! Msimu huu si KAMA ULIVYOZOEA!

Ubongo Kids MPYA inamjenga mwanao, ikimpa fikra komavu zitakazomwezesha kutambua kusudi lake masomoni na maishani!

Njoo nasi Kokotoa, ukajifunze kutumia uwezo na utashi wako kusuluhisha changamoto zinazokukabili ili ufike pale utakapo!

Msimu wa 3 wa Ubongo Kids utakuandaa kifikra, ukichochea uwezo wako wa kung’amua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi.

Ubongo Kids ni mfululizo wa hadithi za kusisimua zilizo katika mfumo wa elimu-burudani kwa ajili ya watoto wa miaka 7 hadi 13, zikitumia nyimbo na maudhui ya Kiafrika kuwafundisha hisabati na sayansi!

Katuni hii mahususi ya elimu inaandaliwa na Ubongo Learning, ambao pia ni watengenezaji wa kipindi murua ya AkiliandMe inayowaandaa watoto wa miaka 3-6 kwa ajili ya kwenda shule!

Tazama Ubongo Kids kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi kupitia TBC1! Pata pia webisodes zetu zote kupitia: http://www.ubongokids.com


Watch video Nyimbo za Sayansi! | Ubongo Kids - elimu burudani wa watoto online without registration, duration hours minute second in high quality. This video was added by user Ubongo Kids Kiswahili 23 June 2017, don't forget to share it with your friends and acquaintances, it has been viewed on our site 4,734,783 once and liked it 6.8 thousand people.