Jinsi ya kufanya Simu itunze Chaji mda Mrefu | how to Increase battery life

Published: 22 May 2023
on channel: MPARADISSO MEDIA Tech
3,782
35

Jinsi ya kufanya simu itunze charge kwa mida mrefu.

Wengi wetu tumekua tukizitolea malalamiko simu zetu kuto tunza chaji kwa muda mrefu, leo nimewaletea njia itayokusaidia kuifanya sim yako itunze chaji kwa mida mrefu.

Ili kusaidia simu yako itunze chaji kwa muda mrefu, unaweza kuzingatia Mambo yafuatazo:

1. Punguza mwangaza wa skrini: Skrini inatumia nguvu nyingi, hivyo kupunguza mwangaza unaweza kusaidia chaji kutoisha kwa haraka. Weka mwangaza wa skrini kwenye kiwango cha chini kinachoweza kukufaa na ikiwezekana tumia mwangaza wa Automatic.
kaitka Auto brightness  ambapo katika simu za android kupata sehemu hii unaenda katika mpangilio (settings )kisha unachagua display ambayo ukifungua ndani yake basi utakutana sehemu ya kupunguza au kuongeza mwana wa simu.

2. Weka muda mfupi wa kuzima skrini: Kupunguza muda ambao simu inasubiri kabla ya kuzima skrini inaweza kusaidia kuokoa chaji. Weka muda mfupi wa kuzima skrini kwenye mipangilio ya simu yako ili kuzuia skrini isibaki wazi bila sababu.

3. Zima Wi-Fi, Bluetooth, na GPS: Huduma kama Wi-Fi, Bluetooth, na GPS hutumia nguvu nyingi za betri. Ikiwa hazitumiki, zima huduma hizo ili kupunguza matumizi ya nguvu na kusaidia betri itunze chaji kwa muda mrefu.
Hakikasha kila wakati ambao hautumii WiFi basi iwe imezimwa katika simu yako maana huchangia kumaliza chaji kwa kiasi kikubwa.

4. weka "Battery Saver": kila sim Ina mode ya battery saver kuhakikisha program zinazotumia nguvu kubwa zinazimwa automatically. Weka simu yako kwenye mode ya Battery Saver" unapokuwa na haja ya kuongeza maisha ya betri. Modes hizi zinazima huduma zisizohitajika na zinapunguza utendaji wa simu ili kuokoa chaji.

5. Funga au zima Background app:a Programu zinazoendelea kufanya kazi nyuma ya pazia zinaweza kutumia nguvu kubwa ya betri.
Simu janja zote zinauwezo wa kuendesha apps zadi ya moja  yaani unaweza kucheza game huku unasikiliza mziki, pia unapokea SMS za whatsApp, na notification kutoka app mbalimbali.
app ambayo inaendelea kufanyakazi ikiwa umefungua app nyingine kitaalamu ni background app na huchangia kumaliza chaji kwa haraka.

6. Tumia mawasiliano ya data ya chini: Matumizi ya data ya juu yanaweza kusababisha matumizi ya nguvu ya betri kuisha haraka, hasa pale mtandao unapoyumbahulazimika kutumia nguvu kubwa kutafuta mtandao.
Ikiwa unaweza, tumia mawasiliano ya data ya chini kama 2G au 3G badala ya 4G au 5G wakati hauhitaji kasi kubwa ya intaneti. basi nguvu ya battery itadumu mda mrefu.

7. Punguza sauti ya simu: sauti za simu pia hutumia nguvu kubwa. pindi unasikiliza mziki nakushauli weka sauti ya chini ili kusaidia kutunza chaji,
Punguza kiwango cha sauti na jaribu kutumia sauti za chini au kusikiliza kupitia headphone badala ya kusikiliza sauti kupitia spika za simu.

8. Ondoa programu za kukula chaji: Angalia programu zako na ondoa programu zisizohitajika au zinazokula chaji kwa kiasi kikubwa. mm

9. Punguza kutumia simu kwa mda mrefu

Hizo ni baadhi ya njia ambazo zitasaidia sim zetu kutunza chaji kwa muda mrefu. Jaribu kufuata ushauri nilioutoa kisha utuambie ni kwa kiasi gani chaji imeongezeka imeongezeka kukaa katika simu.


Watch video Jinsi ya kufanya Simu itunze Chaji mda Mrefu | how to Increase battery life online without registration, duration hours minute second in high quality. This video was added by user MPARADISSO MEDIA Tech 22 May 2023, don't forget to share it with your friends and acquaintances, it has been viewed on our site 3,78 once and liked it 3 people.